Islamic Vault
74

Al-Muddaththir

سورة المدثر

The Cloaked One56 ayat Makkiyyah

Translated by Ali Muhsin Al-Barwani

بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ

1

بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ يَا أَيُّهَا الْمُدَّثِّرُ

Ewe uliye jigubika!

2

قُمْ فَأَنْذِرْ

Simama uonye!

3

وَرَبَّكَ فَكَبِّرْ

Na Mola wako Mlezi mtukuze!

4

وَثِيَابَكَ فَطَهِّرْ

Na nguo zako, zisafishe.

5

وَالرُّجْزَ فَاهْجُرْ

Na yaliyo machafu yahame!

6

وَلَا تَمْنُنْ تَسْتَكْثِرُ

Wala usitoe kwa kutaraji kuzidishiwa.

7

وَلِرَبِّكَ فَاصْبِرْ

Na kwa ajili ya Mola wako Mlezi, subiri!

8

فَإِذَا نُقِرَ فِي النَّاقُورِ

Basi litapo pulizwa barugumu,

9

فَذَٰلِكَ يَوْمَئِذٍ يَوْمٌ عَسِيرٌ

Siku hiyo, basi, itakuwa siku ngumu.

10

عَلَى الْكَافِرِينَ غَيْرُ يَسِيرٍ

Kwa makafiri haitakuwa nyepesi.

11

ذَرْنِي وَمَنْ خَلَقْتُ وَحِيدًا

Niache peke yangu na niliye muumba;

12

وَجَعَلْتُ لَهُ مَالًا مَمْدُودًا

Na nikamjaalia awe na mali mengi,

13

وَبَنِينَ شُهُودًا

Na wana wanao onekana,

14

وَمَهَّدْتُ لَهُ تَمْهِيدًا

Na nikamtgenezea mambo vizuri kabisa.

15

ثُمَّ يَطْمَعُ أَنْ أَزِيدَ

Kisha anatumai nimzidishie!

16

كَلَّا ۖ إِنَّهُ كَانَ لِآيَاتِنَا عَنِيدًا

Hasha! Kwani hakika yeye alikuwa akizifanyia inadi Aya zetu!

17

سَأُرْهِقُهُ صَعُودًا

Nitamtesa kwa mateso yasio wezekana.

18

إِنَّهُ فَكَّرَ وَقَدَّرَ

Kwani hakika yeye alifikiri na akapima.

19

فَقُتِلَ كَيْفَ قَدَّرَ

Basi ameangamia! Vipi alivyo pima!

20

ثُمَّ قُتِلَ كَيْفَ قَدَّرَ

Tena ameangamia! Vipi alivyo pima!

21

ثُمَّ نَظَرَ

Kisha akatazama,

22

ثُمَّ عَبَسَ وَبَسَرَ

Kisha akakunja kipaji, na akanuna.

23

ثُمَّ أَدْبَرَ وَاسْتَكْبَرَ

Kisha akaipa kisogo haki, na akatakabari.

24

فَقَالَ إِنْ هَٰذَا إِلَّا سِحْرٌ يُؤْثَرُ

Na akasema: Haya si chochote ila ni uchawi ulio nukuliwa.

25

إِنْ هَٰذَا إِلَّا قَوْلُ الْبَشَرِ

Haya si chochote ila kauli ya binaadamu.

26

سَأُصْلِيهِ سَقَرَ

Nitakuja mtia kwenye Moto wa Saqar.

27

وَمَا أَدْرَاكَ مَا سَقَرُ

Na nini kitakujuulisha ni nini huo Moto wa Saqar?

28

لَا تُبْقِي وَلَا تَذَرُ

Haubakishi wala hausazi.

29

لَوَّاحَةٌ لِلْبَشَرِ

Unababua ngozi iwe nyeusi.

30

عَلَيْهَا تِسْعَةَ عَشَرَ

Juu yake wapo kumi na tisa.

31

وَمَا جَعَلْنَا أَصْحَابَ النَّارِ إِلَّا مَلَائِكَةً ۙ وَمَا جَعَلْنَا عِدَّتَهُمْ إِلَّا فِتْنَةً لِلَّذِينَ كَفَرُوا لِيَسْتَيْقِنَ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ وَيَزْدَادَ الَّذِينَ آمَنُوا إِيمَانًا ۙ وَلَا يَرْتَابَ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ وَالْمُؤْمِنُونَ ۙ وَلِيَقُولَ الَّذِينَ فِي قُلُوبِهِمْ مَرَضٌ وَالْكَافِرُونَ مَاذَا أَرَادَ اللَّهُ بِهَٰذَا مَثَلًا ۚ كَذَٰلِكَ يُضِلُّ اللَّهُ مَنْ يَشَاءُ وَيَهْدِي مَنْ يَشَاءُ ۚ وَمَا يَعْلَمُ جُنُودَ رَبِّكَ إِلَّا هُوَ ۚ وَمَا هِيَ إِلَّا ذِكْرَىٰ لِلْبَشَرِ

Na hatukuwafanya walinzi wa Motoni ila ni Malaika, wala hatukuifanya idadi yao hiyo ila kuwatatanisha walio kufuru, wapate kuwa na yakini walio pewa Kitabu, na wazidi Imani wale walio amini, wala wasiwe na shaka walio pewa Kitabu na Waumini, na wapate kusema wenye maradhi katika nyoyo zao na makafiri: Mwenyezi Mungu amekusudia nini kwa mfano huu? Ndio kama hivyo Mwenyezi Mungu humwacha apotee amtakaye, na humwongoa amtakaye. Na hapana yeyote anaye jua majeshi ya Mola wako Mlezi ila Yeye tu. Na haya si chochote ila ni ukumbusho kwa binaadamu.

32

كَلَّا وَالْقَمَرِ

Hasha! Naapa kwa mwezi!

33

وَاللَّيْلِ إِذْ أَدْبَرَ

Na kwa usiku unapo kucha!

34

وَالصُّبْحِ إِذَا أَسْفَرَ

Na kwa asubuhi inapo pambazuka!

35

إِنَّهَا لَإِحْدَى الْكُبَرِ

Hakika huo Moto ni katika mambo yaliyo makubwa kabisa!

36

نَذِيرًا لِلْبَشَرِ

Ni onyo kwa binaadamu,

37

لِمَنْ شَاءَ مِنْكُمْ أَنْ يَتَقَدَّمَ أَوْ يَتَأَخَّرَ

Kwa anaye taka miongoni mwenu kutangulia au kuchelewa.

38

كُلُّ نَفْسٍ بِمَا كَسَبَتْ رَهِينَةٌ

Kila nafsi imo rahanini kwa mabaya iliyo yachuma.

39

إِلَّا أَصْحَابَ الْيَمِينِ

Isipo kuwa watu wa kuliani.

40

فِي جَنَّاتٍ يَتَسَاءَلُونَ

Hao watakuwa katika Mabustani, wawe wanaulizana

41

عَنِ الْمُجْرِمِينَ

Khabari za wakosefu:

42

مَا سَلَكَكُمْ فِي سَقَرَ

Ni nini kilicho kupelekeni Motoni?

43

قَالُوا لَمْ نَكُ مِنَ الْمُصَلِّينَ

Waseme: Hatukuwa miongoni walio kuwa wakisali.

44

وَلَمْ نَكُ نُطْعِمُ الْمِسْكِينَ

Wala hatukuwa tukiwalisha masikini.

45

وَكُنَّا نَخُوضُ مَعَ الْخَائِضِينَ

Na tulikuwa tukizama pamoja na walio zama katika maovu.

46

وَكُنَّا نُكَذِّبُ بِيَوْمِ الدِّينِ

Na tulikuwa tukiikanusha siku ya malipo.

47

حَتَّىٰ أَتَانَا الْيَقِينُ

Mpaka yakini ilipo tufikia.

48

فَمَا تَنْفَعُهُمْ شَفَاعَةُ الشَّافِعِينَ

Basi hautawafaa kitu uombezi wa waombezi.

49

فَمَا لَهُمْ عَنِ التَّذْكِرَةِ مُعْرِضِينَ

Basi wana nini hata wanapuuza onyo hili?

50

كَأَنَّهُمْ حُمُرٌ مُسْتَنْفِرَةٌ

Kama kwamba wao ni mapunda walio timuliwa,

51

فَرَّتْ مِنْ قَسْوَرَةٍ

Wanao mkimbia simba!

52

بَلْ يُرِيدُ كُلُّ امْرِئٍ مِنْهُمْ أَنْ يُؤْتَىٰ صُحُفًا مُنَشَّرَةً

Ati kila mmoja katika wao anataka apewe nyaraka zilizo funuliwa.

53

كَلَّا ۖ بَلْ لَا يَخَافُونَ الْآخِرَةَ

Hasha! Kwani wao hawaiogopi Akhera?

54

كَلَّا إِنَّهُ تَذْكِرَةٌ

Hasha! Kwa hakika huu ni ukumbusho!

55

فَمَنْ شَاءَ ذَكَرَهُ

Basi anaye taka atakumbuka.

56

وَمَا يَذْكُرُونَ إِلَّا أَنْ يَشَاءَ اللَّهُ ۚ هُوَ أَهْلُ التَّقْوَىٰ وَأَهْلُ الْمَغْفِرَةِ

Na hawatakumbuka isipo kuwa Mwenyezi Mungu atake. Uchamngu ni kwake Yeye, na msamaha ni wake Yeye.

Islamic Vault

Quran Explorer

Sumber dalam talian yang komprehensif untuk membaca dan mengkaji Al-Quran dengan pelbagai terjemahan, transliterasi, dan bacaan audio daripada qari terkenal.

Kitab ini tidak ada keraguan padanya, petunjuk bagi orang-orang yang bertakwa.

Al-Quran 2:2

Ciri-ciri

  • Bacaan Audio
  • Pelbagai Terjemahan
  • Transliterasi
  • 114 Surah
  • 6,236 Ayat

© 2026 Islamic Vault. Hak cipta terpelihara.

Dibina dengan penghormatan dan ketelitian untuk Kitabullah

Dibangunkan oleh Medita Development

Penafian: Walaupun kami berusaha untuk ketepatan, sila sahkan maklumat agama penting dengan ulama Islam dan sumber yang sahih. Platform ini adalah untuk tujuan pendidikan.